Advertise with Us

Advertise with Us

DHall

DHall

Pages

October 17, 2012

-}i{- BREAKING NEWS- KIONGOZI WA KIKUNDI CHA UAMSHO ZANZIBAR ATEKWA NYARA

Mpaka sasa Kiongozi huyo wa Uamsho hajulikani alipo- Hali ni tete huko Zanzibar
Jengo la maskani ya CCM-Kisonge ambalo limechomwa moto na wafuasi wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa Uamsho.

Kwa mujibu wa Katibu wake, Abdallah Said Ally, amesema alikuwa na dereva wake maeneo ya Michenzani akitokea nyumbani kwake Mbuyuni, ndipo akakutana na gari moja ambalo dereva halifahamu na akashuka mwenyewe kwenye gari lake na kuingia katika hilo gari na kuanzia hapo hadi sasa hajulikani alipo.

Katibu huyo wa Uamsho na wenzake wamekuwa katika juhudi za kutuliza jazba za wafuasi wao na sasa wanawasiliana na polisi kujua alipo kiongozi wao.

Sheikh Farid alipotea muda ule ule ambao inadaiwa mwenzake [Sheikh Ponda] alikamatwa mida ya saa 5 usiku wa kuamkia leo.


Pichani ni hali halisi inayoendelea huko Zanzibar ambako wafuasi wa Uamsho wanaandamana na kufanya vurugu na uharibifu wa mali na vitu kadhaa ambavyo mpaka sasa thamani halisi ya mali na vitu vilivyoharibika haijaweza kujulikana mara moja.

Maisha Times itaendelea kuwapasha habari kadiri zitakavyoendelea kupatikana.

No comments:

Post a Comment