Advertise with Us

Advertise with Us

DHall

DHall

Pages

November 22, 2012

-§- Mwisho wa Beef ya Floyd Mayweather na 50 Cent ni kuzichapa jukwaani December13-14!

 Wakati Bongo Beef za wasanii zikilenga zaidi katika kutiana hasara na hata kuangamizana kwa wenzetu Beef zinafanyika kwa faida!
50 Cent & Floyd Mayweather, Jr.

50 Cent & Floyd Mayweather, Jr. 

 Pacquiao and 50 Cent

Nadhani kwa wale mnaofuatilia kwa karibu habari za nje mtakuwa mnajua Beef inayoendelea kati ya Rapper Maarufu 50Cent na Bondia maarufu wa Uzito wa WBC welterweight WBA (Super) light middleweight champion na WBC diamond belt; Floyd Mayweather, Jr. wote wakiwa ni raia wa Marekani.
Habari zaidi zinasema kwamba 50 Cent na bingwa wa ndondi Floyd Mayweather, Jr wamepewa ofa ya dola milioni 10 iwapo watapanda ulingoni kuzichapa ili kumaliza beef yao.
Maswahiba hao wa zamani wamepewa ofa hiyo ambapo kila mmoja atapewa dola milioni 5.

50 Cent na Floyd Mayweather mwanzoni walikuwa marafiki wa karibu lakini wamejikuta wakiingia katika uadui baada ya kushindwa kuelewana kwenye masuala ya biashara na kuanza kupigana vijembe kwenye mtandao wa Twitter.

Bilionea Alki David na promoter Damon Feldman wamewapa mastaa hao ofa hiyo ili waingie ulingoni kuzitwanga katika mchezo utakaokuwa na raundi tatu.

David anasema mechi hiyo itaruka live kupitia mtandao wa Filmon.com na Battlecam.com.
Kwa upande wake 50 amesema yupo tayari kuingia ulingoni kwa kuandika jana  kwenye Twitter, “ I'll fight Him dec 14th is too soon. I would need time to get in shape. I'm 204 right now I hit that boy he will see a white light.

Bofya hapa kupata habari zaidi http://www.opposingviews.com/i/sports/boxingmma/floyd-mayweather-vs-50-cent-complete-recap-stupid-beef


No comments:

Post a Comment