Advertise with Us

Advertise with Us

DHall

DHall

Pages

December 11, 2012

-§- TATIZO LA BIASHARA YA MADAWA YA KULEVYA NCHINI SERIKALI INACHANGIA!


Rais jakaya Kikwete na Msanii Ray C wakati msanii huyo alipokwenda ikulu kumsalimu na kumshukuru Rais kwa kumgharamia matibabu yake.

Kama ambavyo vyombo vingi vya habari nchini vilivyoweza kuripoti na kutoa taarifa juu ya uamuzi wa busara wa rais Jakaya Kikwete kumsaidia msanii wa Bongo Flavour "Ray C" gharama za matibabu yaliyotokana na kuathiriwa na matumizi ya dawa za kulevya, binafsi nina hoja tofauti kidogo. Kitendo cha Rais Jk au Serikali yake kwa ujumla kuamua kuwasaidia waathirika wa madawa ya kulevya ilihali Serikali ikishindwa kabisa kudhibiti waingizaji na wauzaji wakubwa wa Madawa ya kulevya nchini hii inakuwaje?

Huu ni mfano hai:
 
Hebu chukulia kitendo cha Mahakama Kuu kutoa dhamana kwa watuhumiwa wa Madawa ya kulevya kinyume kabisa na sheria na hatimae watuhumiwa kutoroka na kutokomea kusikojulikana kinatoa picha gani kwa Wananchi ?¿ habari hii inapatikana katika Gazeti la Jambo Leo la tarehe 11.12.2012. Hawa ni watuhumiwa ambao ni raia wa nchini Pakistani waliokamatwa nchini Tanzania kwa tuhuma za uingizaji wa madawa ya kulevya. Sheria inasema wazi kwamba dhamana itatolewa kwa watuhumiwa ambao thamani ya madawa waliyokamatwa au kujihusisha nayo haizidi Tsh mil.10 lakini hali imekuwa ni kinyume baada ya watuhumiwa hao kupewa dhamana na mahakama ilihali thamani ya madawa waliyokamatwa nayo ikizidi kiwango tajwa na kukiuka vigezo vya kupewa dhamana hilyo.

Ikumbukwe kwamba tangu mwaka 2006 mpaka sasa tayari Rais Jakaya Kikwete  alikuwa ameshakabidhiwa listi kamili ya Vigogo na wafanyabiashara wakubwa wanaojihusisha na biashara hiyo haramu ya madawa ya kulevya lakini tangu kipindi hicho mpaka sasa hakuna hatua zozote za kisheria zilizochukuliwa jambo ambalo limewaacha njia panda wananchi na kushindwa kuelewa kama kweli Serikali ya tanzania na viongozi wake wanayo nia ya kweli ya kuitokomeza kabisa biashara hiyo haramu au la.
 

Habari zaidi : Gazeti la Jambo Leo tarehe 11.12.2012
na http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/257-majina-ya-wauza-madawa-ya-kulevya-kikwete-anayo-18.html

No comments:

Post a Comment